Jumuia
Msukumo wenye kariha kutoka kwa Washiriki
Taasisi, jamii, na familia zilizojiunga na Jukwaa Tendaji la Laudato Si zinapiga hatua kuu kwenye azma ya uhimilivu kamili katika dhati ya moyo wa Laudato Si. Kama sehemu ya kujitolea kwetu kwa pamoja ili kuujenga mustakabali wetu, viongozi vindakindaki wanatafakari kuhusu namna maadili yao yanavyochukuana na Shabaha za Laudato Si na kuzibuni plani za matendo na hatua halisi katika mwaka ujao.
Bofya ili kutazama makala na video kutoka kwa washiriki ambao wanatafakari kuhusu Shabaha za Laudato Si’ na kuzibuni Plani za Laudato Si’.
Ijenge jamii kiasilia
Kuujenga mustakabali bora kunahitaji,”ushiriki ulio hai wa wanajamii wote.” (LS 144) Jukwaa Tendaji la Laudato Si’ hutoa fursa ya wote ili kusaka na kugawana au kushiriki kimawazo, hata hivyo ni moyoni mwake ni jamii kindakindaki zilizomo. Unao uhuru wa kuzitumia nyenzo ili kuukuza uhusiano wa jamii katika eneo lako asilia.
Washirika wa Jukwaa Tendaji la Luadato Si’
Jukwaa Tendaji la Laudato Si’ ni zao la ushirikiano wa kipekee baina ya Wizara ya Ukuzaji wa Maendeleo Muhimu ya Kibinadamu – Vatikani, takriban mashirika mia moja hamsini (200), na watu binafsi kote ulimwenguni.
Makala ya Jamii
“Sote tunaweza kushirikiana kama vyombo vya Mungu vya utunzaji wa vyote alivyoviumba, kila mtu kwa tamaduni zake, tajriba, uhusika na vipaji.” (LS 14)