Wadau Wetu

Washirika wa Jukwaa Tendaji la Luadato Si’

Jukwaa Tendaji la Laudato Si’ ni zao la ushirikiano wa kipekee baina ya Wizara ya Ukuzaji wa Maendeleo Muhimu ya Kibinadamu – Vatikani, takriban mashirika mia moja hamsini (200), na watu binafsi kote ulimwenguni.

Moyo wa ushirikiano huliimarisha Jukwaa Tendaji la Laudato Si’ kwa jumla, hivyo basi kuhakikisha kuwa limejikita katika tajiriba halisi za kimaisha na busara ya jamii asili. Yakini, “ njia mpya zinazoaasisiwa haziwezi kutoshelezwa vyema katika mifumo ya kutoka nje; zinahitaji kuwekewa msingi katika mila asili zenyewe.” (LS 144)
Wizara ya Ukuzaji wa Maendeleo Muhimu ya Kibinadamu inapania kwa wingi wa shukrani kujifundisha kutoka kwa viongozi kindakindaki wa pale na kwa unyenyekevu mkuu itoe mfumo sawa utakaoyapiga jeki maendeleo ya wote kwa jumla.

Miongoni mwa makundi na mashirika mengi ambayo Roho Mtakatifu ameyaunganisha katika amali hii, uongozi wa jumuia zilizoko “pembezoni.” Wakati wa changamoto, walio pembezoni huonyesha “ ubunifu na ukarimu wa kuvutia” na hufuma “ mshikamano wa uhusika na umoja” ambavyo vimekuwa msingi muhimu katika kustawisha/kukuza programu hii.

Unganika katika Roho Mtakatifu

Jukwaa Tendaji la Laudato Si’ ni zao la juhudi za ushirikiano. Mashirika na watu binafsi kutoka kila upande wa ulimwengu wamechangia katika makuzi yake.

Maono mapevu ya washirika yamesaidia kuhakikisha kuwa mfumo wa kilimwengu wa jukwaa hili unakidhi mahitaji ya jumuia za wenyeji.

Mfadhili

Halmashauri Elekezi

Wanakundi wafanyakazi

“Sote tunaweza kushirikiana kama vyombo vya Mungu vya utunzaji wa vyote alivyoviumba, kila mtu kwa tamaduni zake, tajriba, uhusika na vipaji.” (LS 14)

Jiandikishe