Wanachama Maria na Gianni Salerno kwa ushirikiano huliongoza kundi la harakati zinazohusu familia za Jukwaa Tendaji la Laudato Si’. Kote ulimwenguni, Shirika la Focalare, linahuisha Laudato Si’ miongoni mwa jamii kindakindaki, kubwa kwa ndogo.
Huko Myanmar, vigori wa Focolare wanaziokota taka za sandarusi kutoka vijiani na kuzipeleka kwa wakarabati wanaozibadili taka hizo kuwa bidhaa za kazi pendezi ya mikono mathalan kwa kufumwa, kusukwa, vikapu na nyinginezo za kisanaa.Tazama zaidi kwenye video hii hapa.
Afrika Mashariki, Kijana mhandisi barobaro Mwitaliano amewasaidia wanajamiii kutoka nchi za Rwanda , Uganda na Congo katika kuanzisha na kuendeleza miradi ya kawi mataifani humo. Anaelezea namna uhusiano wake na jamii hizo unavyoimarika na kuipa mantiki kazi yake. Tazama zaidi kwenye video hii hapa.
Ufilipino, Profesa au fundi Msanifu-ujenzi katika Chuo Kikuu cha De La Salle anawaongoza wanafunzi wake katika mradi wa kusafisha kwa kuondoa taka kwenye Mto wa Manila Pasig.Wakazi wa nyumba za kufaraguliwa waishio kwenye kingo za mto huo ndio kiungo muhimu kwa ushirika wao katika zoezi hili. Tazama zaidi kwenye video hii hapa.
Familia ya Salerno imejitolea mhanga katika kuujenga mustakabali bora kwa pamoja na wanachama wote wa Shirika la Focolare na washirika wa Jukwaa Tendaji la Laudato Si’ ulimwenguni kote. Umealikwa kuzizingatia hatua zijazo katika safari yako kwa kuzitumia nyenzo kwenye tovuti ya Jukwaa Tendaji la Laudato Si’.