Shabaha za Laudato Si’
Kuhusu Laudato Si’
Jukwaa Tendaji la Laudato Si’ inaliwezesha Kanisa Ulimwenguni na wote wa nia njema kuitikia wito wa Laudato Si‘ wa Waraka wa Baba Mtakatifu Fransisko kuhusu utunzaji wa dunia – makao yetu sote.
Kwa kutalii mafundisho ya kale ya imani yetu kwa kuegemea migogoro ya kisasa ya kiikolojia, Laudato Si’ inatufundisha kuwa “ kila kitu kimefungamanishwa.” (LS 91) Kwa kuwa uhusiano wetu na Muumba Mtakatifu umetelekezwa, mahusiano ya kibinadamu pia yamesambaratika, na ulimwengu wetu umezidisha hari, usiokuwa na utulivu toshelevu na usio hai. Hatimaye, sote tunateseka, na wale wachochole sana na wasiokingwa vilivyo huteseka zaidi ya wote. Tunakabiliwa na “ janga kubwa ambalo ni la kijamii na kimazingira.” (LS 139)
Matumaini yapo. Papa Fransisko anatuita kukuza “ ufahamu wa kimapendo” wa makao tunayoshiriki na kutumikiza maadili tunayokumbatia kwa dhati ya moyo. (LS 220)
Kwa kusimama kwenye msingi imara wa “ viini vitatu muhimu na vyenye kuunganika kimahusiano: Uwepo wa Mungu, na wa jirani, na wa dunia yenyewe,” tunajitolea mhanga kung’oa nanga kwenye mwendo mrefu wa kupyaishwa” (LS 66, 202) Tunajinyakulia mahali stahili yetu katika “ mpangilio na nguvu mpya” kuwa Muumba wetu alitawaza, na kwa wepesi tunaingilia mbinu mpya za kuishi kwa “ ubunifu na uchangamfu mkuu.” (LS 221, 220)
Shabaha za Laudato Si’
Kwa taarifa zaidi, umeitwa kuipitia upya orodha kamili ya shabaha na mswada wa orodha yenye hatua zilizopendekezwa hapa.
“Lengo letu si kukusanya maarifa mengi ya kutosheleza kiu ya utafiti, bali ni kujifahamisha kwa undani, kujaribu kubadilsha yanayofanyika ulimwenguni ili kuwa masumbuko yetu binafsi na kugundua anayoweza kufanya kila mmoja wetu kuyahusu.” (LS 19)