Mei 2009, Halibari Aila ilisababisha maafa ya ajabu huko India Bangladesh, na kusababisha vifo mia tatu thelathini na tisa (339) na kuwahamisha nyumbani kwao zaidi ya watu milioni moja. Ongezeko la nguvu, kasi na muda wa baadhi ya dhoruba hizi za tropiki linaweza kuhusishwa na mabadiliko ya hali ya anga, kwa kuwa maji yenye joto ya bahari huzipa nguvu zaidi dhoruba zipitiazo kwayo.
Katika hali ilivyokuwa kutokana na Halibari Aila,Seva Kendra ilichukua hatua.
Seva Kendra Calcutta ndicho Kituo rasmi cha Huduma za Jamii katika Dayosisi kuu ya Calcutta. Padre Franklin Menezes, Mkurugenzi wa Seva Kendra, ni mshiriki wa Jukwaa Tendaji la Laudato Si’. Shughuli za Seva Kendra ni kivutio kikuu kwa wengi ndani na nje ya eneo hili.
Nishati madhubuti na safi kunururisha
Seva Kendra imeanzisha namna anuwai za vifurushi vya nishati nururifu ili kuboresha maisha ya wakazi wa pale, kwa kujumuisha taa za nishati ya jua pamoja na mafunzo ya kina na elimu.
Katika maeneo yaliyojaa ukabila ya Parokia ndogo ya Midnapore, mradi wa kunururisha wa Seva Kendra umekuwa mfumo mkuu, umewapa mafunzo mafundi mia tano na sita(506) ambao walikuwa si wasomi bali wanawake wenye kujawa na ukabila. Kazi ya Programu ya mafundisho haya ya nishati ya jua huwa ni namna kuu ya kuzibua riziki na fursa bora kwa wanawake hawa. Hadi sasa, shirika hili limewekeza takriban vituo arubaini (40) vya kutoa mafunzo na kuzalisha kawi katika vijiji arubaini (40) vilivyotengwa, pia limekuza njia nane kuu za uuzaji ambazo wafanyakazi wake ni mafundi waliopewa mafunzo, na kuuza zaidi ya taa alfu thelathini (30,000) za nishati ya jua.
Kwa kuzidi kuwekea msingi shughuli zake katika Parokia ndogo ya Midnapore, Seva Kendra imesababisha kuwapo kwa zaidi ya vituo ishirini (20) vya kutoa mafunzo katika Dayosisi ya Bengal Magharibi na hata mbali zaidi kufikia Myanmar na Tailandi, na hivyo kuwaletea matuamaini halisi watu wa ndani na nje ya mipaka ya hii dayosisikuu.
Mradi wa kunururisha wa Seva Kendra sio tu wa pekee katika programu hii. Imeweza pia kuelekeza mabadiliko kutoka kwenye balbu zenye nyaya ndani yake hadi kwa zile za LED nyumbani kote katika maeneo haya yaliyofukarika na kujawa na ukabila. Taa hizi husaidia kupunguza gharama za kawi, na kuundwa kwazo hushusha gharama kwa hiyo kutoa nafasi ya ajira kwa wakazi hawa. Taasisi nyingi katika Dayosisikuu ya Calcutta pia zimeingilia matumizi ya taa za LED, na hivyo basi kusaidia katika kutoa nafasi bora za ajira zaidi huku zikihifadhi nishati.
Viambajengo vya hadhi na heshima
Mbali na nishati ya mwanga, Seva Kendra imebuni mifumo ya kuwasaidia watu kuishi maisha yenye hadhi na ya heshima kupitia utoaji na upatikanaji wa mahitaji ya msingi.
Shirika hili limeweka mifumo ya nishati jua kwenye mapaa katika zaidi ya taasisi mia moja (100) na mifumo ya kukanza maji katika zaidi ya taasisi hamsini (50). Katika kisiwa cha mbali cha Satjelia, shirika hili limeweka paneli za nishati ya jua na mtambo mdogo wa kinu cha upepo ili kuwapa umeme wakazi wa nyumba kama nne hivi usiku na mchana. Safu ya sola zenye kipimo cha kilowati 100 ndiyo hutumika kutoa umeme katika ofisi za shirika lenyewe.
Wanakijiji wa Parokia ndogo ya Midnapore wanaweza kutulia na kupunguza muda utumikao katika kutafuta kuni na majani kwa kutumia majiko yaliyoundwa na kuboreshwa zaidi na Seva Kendra.
Kwa watu wasioweza kupata maji safi, Seva Kendra imeunda aina ya machujio ya “bio-sand” ambayo ni mfumo uliotoholewa kwa mahitaji yao ili kuyachujia maji, hii ni njia maarufu ya kukata gharama na rahisi kudumisha. Elimu kuhusu machujio haya imefanywa katika maeneo ya Kaskazini 24 ya wilaya ya Parganas, ambako kuna viwango vya juu vya aseniki.
Hatimaye, Seva Kendra imekuza mifumo ya kilimo inayomilikiwa na wakazi asilia ili kuwapa lishe bora yenye afya, kawaida chakula hiki hukuzwa bila ya kemikali. Programu zake zimewasaidia watu kuanzisha vishamba vidogo, kuhifadhi mbegu za asili, na kusoma mbinu himilivu za kilimo.Programu zake za Elimu kwa Wakulima zimehusisha nyumba tatu za watoto zinazoendeshwa na serikali na mabweni ishirini na mawili (22)
Yamkini, la kuajabisha hapa ni, kupitia kwa kazi murua za Seva Kendra, wanawake elfu moja (1000) wameimarishwa kwa kilimo hai, yaani; ukulima usiotumia kemikali, na kuwapa si maarifa tu na mafundisho muhimu bali pia mbegu na miche ili kufutilia mbali hasara walizopata wakati wa Kimbunga cha Amphan kilicholeta maafa mengi mwaka wa 2020.
Shughuli za Seva Kendra ni ithibati kamili ya nguvu za matumaini wakati wa mashaka makuu. Washirika wa Jukwaa Tendaji la Laudato Si’ wanajumuika pamoja kwa kuyajenga maisha bora ya baadaye. Umealikwa kuzizingatia hatua zijazo katika safari yako kwa kuzitumia nyenzo kwenye tovuti ya Jukwaa Tendaji la Laudato Si’.