Plani za Laudato Si’
Matendo yetu ni muhimu. Matendo haya “huathiri ulimwengu unaotuzunguka moja kwa moja na kwa kiasi kikubwa.” (LS 211) Taasisi, jamii, na familia ambazo zimejiunga na Jukwaa Tendaji la Laudato Si’ zinachukua hatua kwa mujibu wa Plani zao za Laudato Si’.
Kwa kutumia mwongozo na mapendekezo yaliyotolewa kwa moyo wa huduma kwa wote wajiungao nasi, washiriki hao wameorodhesha hatua zijazo katika safari zao kwenye uhimilivu kamili kwa dhati ya moyo wa Laudato Si’. Wanazitoa plani zao kwa ukarimu mkuu kwako, kutoa mifano halisi ya namna msukumo wa kariha huishia kuwa matendo.