Nyenzo
Katika Laudato Si’, Baba Mtakatifu Fransisko anatualika kwa kusudi la “kugundua anachoweza kufanya kila mmoja wetu” huku tukiujenga mustakabali bora wa maisha yetu pamoja. (LS 19) Kuitika wito wa Laudato Si’ humaanisha kuzikubali njia mpya za kuishi, huku ufahamu wetu kuhusu maingiliano mbalimbali ukizidi kukua na kuwakilishwa na matendo halisi.
Huku ukisaka taarifa kuhusu mbinu za utekelezaji, umealikwa kutumia nyenzo zifuatazo. Utaweza kupata utaalamu halisi na amilifu ambao utakupiga jeki katika maendeleo yako kwenye Shabaha za Laudato Si’. Nyenzo hizi zimetolewa kwa ukarimu na jamii anuwai za mashirika ya Kikatoliki na wambia wengineo, wote wakifanya kazi kwa pamoja alimradi kuihuisha ruwaza ya Laudato Si’.
Wewe ni mwenzetu katika kuujenga mustakabali wetu, hivyo basi, umealikwa ili kuzitumia nyenzo zozote ziwazo zile miongoni mwa ulizopewa hapa huku ukiendelea hatua kwa hatua, sako kwa bako na safari tunayoshiriki pamoja kwenye uhimilivu kamili kwa moyo wa ikolojia fungamano.
Tafadhali tumia vitufe vya Tafuta na Vichujaji vifuatazo ili kusakura nyenzo.
“Ni kwa kupalilia maadili razini pekee wanadamu wataweza kujitolea mhanga kiikolojia” (LS 211)