Makala ya Jamii

Muungano wa Kikatoliki wa Afya Hutunza Mwili na Roho

Posted 7 June 2021

 Video kwa hisani ya Muungano wa Kikatoliki wa Afya, Marekani.

Zaidi ya mmoja kwa saba ya wagonjwa nchini Marekani hushughulikiwa na hospitali ya Kikatoliki, hii huibua fursa za thamani isiyokadirika ya kugawana na kushiriki mapendo ya uponyaji wa Mwokozi wetu. Muungano wa Kikatoliki wa Afya, Marekani husaidia vituo vya afya ambavyo huwatunza wagonjwa hawa, hivyo kuikubali ruwaza jumlishi ya uponyaji unaokita mizizi katika utoaji wa huduma bora zaidi za kiafya kwa watu na jamii kimawazo, kimwili na kiroho. 

Muungano wa Kikatoliki wa Afya, Marekani huhudumia hospitali mia sita (600) na zaidi ya vituo vingine alfu moja na mia sita (1600) vya afya, pia ni mshirika wa maendeleo katika Jukwaa Tendaji la Laudato Si’. Mtazamo wake kuhusu mahitaji na tajriba au uzoefu katika utoaji wa huduma za afya huko Marekani huyaboresha maendeleo na makuzi ya jukwaa hili kwa jumla. 

Video iliyotangulia ( ipo katika Lugha ya Kiingereza) inaelezea vizuri sana simulizi kuhusu namna Muungano wa Kikatoliki wa Afya, Marekani na wanachama wake wanavyoyashirikisha mafundisho ya Kikatoliki kuhusu Uumbaji katika amali wazifanyazo. 

Umealikwa kwa ukarimu ili kuutambua wito wako wa kushiriki katika muungano huu. Zitumie nyenzo kwenye Jukwaa Tendaji la Laudato Si’ ili kujifundisha mengi zaidi.