Kuhusu Jukwaa Tendaji la Laudato Si’
Tumikiza Mpango wa Laudato Si’ wa makao yetu ya pamoja katika vitendo. Kuanzia papo hapo ulipo. Kuanzia leo hii.
Jukwaa Tendaji la Laudato Si’ ni nafasi ya pamoja ambapo Kanisa linakuza mwitiko wa ujasiri na tendaji kwa shida ya kiikolojia, ambayo imeonyeshwa kwa dharura katika waraka wa Papa Fransisko Laudato Si’. Jukwaa Tendaji la Laudato Si’ hukupa vifaa vya kuchukua hatua sasa, wakati ni kwa “dharura na muhimu.” (LS 57)
Misingi ya Jukwaa Tendaji la Laudato Si’
Jiandikishe sasa ili upate usaidizi kamili wa safari yako kuelekea ikolojia fungamano.
Maswali? Tazama ukurasa wetu wa maswali yaulizwayo mara kwa mara, ikiwa ni pamoja na fomu ya kututumia barua pepe ikiwa hutapata jibu unalotafuta.
MIONGOZO
Tunapozidi kuchunguza kwa undani safari hii ya Laudato Si’, athari za makutano yetu na Yesu zinakuwa dhahiri katika uhusiano wetu na ulimwengu unaotuzunguka. (LS 217) Mipango ya Laudato Si’ itaipiga jeki safari ya jamii yako kwenye ikolojia hii fungamano.
Jukwaa hutoa
- Miongozo ya Mipango ya Laudato Si' na violezo vya taasisi yako, jumuiya, au familia ili kupanga jinsi ya kuchukua hatua
- Mipango ya Tafakari na violezo vinavyounganisha maadili yako ya msingi na Malengo ya Laudato Si' na kutumika kama mwanga kwa wengine
NYENZO
Muumba wetu anatuita sote ili kuanza maisha mapya ambayo ni “mazuri, halali na yanayopendeza.” (LS 205) Tunajitolea kuchukua hatua kwa pamoja madhali ni “muhimu na inapaswa kuwa hivyo.”
Jukwaa hutoa
- Tathmini ya kibinafsi, iliyoundwa kulingana na hali yako ya kipekee, ili kukusaidia kuelewa mahali unaposimama leo
- Vitendo vinavyopendekezwa, vilivyoundwa kulingana na mahitaji yako ya kipekee, ili kuleta athari kubwa katika ikolojia muhimu
MSAADA
Safarini tutakumbwa na changamoto. Mashauri na msaada wa ndugu zetu katika Kristo vitatupa nguvu kadri tutakavyoendelea na safari. “ Tuliumbiwa mapendo,” na uhusiano imara utatunawirisha popote Roho Mtakatifu atakapotuelekeza. (LS 58)
Jukwaa hutoa
- Nyenzo katika lugha, sekta na Shabaha za Laudato Si' ili kutoa mwongozo wa ulimwengu halisi kutoka kwa washirika ambao ni wataalamu katika kuchukua hatua
- Miunganiko na washiriki wengine na Vikundi Kazi vya kisekta ili kushiriki maslahi na changamoto
- Matukio yanayotolewa na jumuiya mbalimbali za washirika mtandaoni na katika maeneo duniani kote.
Idara zinazohudumiwa
Maswali yaulizwayo mara kwa mara
Jukwaa Tendaji la Laudato Si’ hutoa msaada wa kina safari hii kwenye ikolojia fungamano kama taasisi, jamii, au familia. Sehemu hii inatoa taarifa amilifu na mfano wa istilahi za kawaida.
“Ipo sababu kutumaini kuwa ubinadamu katika mwanzo wa karne ya ishirini na moja utakumbukwa kwa ukarimu wake katika kutekeleza majukumu yake makuu.” (LS 165)