Tunapoianzisha safari hii ya mabadiliko katika uhimilivu kamili kwa moyo wa Laudato Si’, Jukwaa Tendaji la Laudato Si’ lina furaha kutoa taarifa za hivi karibuni zaidi kuhusu hatua zijazo katika safari hii.
Karibu mashirika ya wambia mia mbili (200) yamekuwa yakifanya kazi kwa pamoja ili kulijenga Jukwaa Tendaji la Laudato Si’ , na tayari jamii kote ulimwenguni zinatoa ahadi zao za moyo ili kuuitika wito wa Laudato Si’ kwa kuutambua na kuutekeleza mpango amilifu kwa msaada wa Mwongozo wa Plani za Laudato Si’.
Taratibu za kisinodi za kulikuza Jukwaa Tendaji la Laudato Si’ zimekuwa zenye kunawiri mno. Ushirikiano wa kiuongozi wa makundi ya wanachama umezua mageuko na maenezi ya mradi huu, na katika majuma ya hivi karibuni, tumehisi kwamba Roho Mtakatifu anawaalika Wanajukwaa Tendaji la Laudato Si’ kuyaendeleza mazungumzo endelevu yaliyomo miongoni mwa washirika anuwai wanaohusika.
Kama njia ya kuuitika wito, tarehe ya usajili wa familia yako, kundi la wanajamii, au taasisi yako, ya kuibuni Plani yako ya Kilaudato Si’ imeongezwa hadi tarehe 14, Novemba, Siku ya Maombi kwa Wanyonge Ulimwenguni.
Makundi mengi tayari yapo vizuri katika kuzibuni Plani zao za Kilaudato Si’, huku wengine wakiwa katika hatua zao za kwanza kwenye safari ya “,mabadiliko ya kiikolojia.” Tunayo matumaini kuwa kwa kutoa nyenzo za ziada mnamo mwezi wa Novemba, badala ya ule wa Oktoba, kutatoa nafasi murua katika mchakato mzima wa ushirikiano unaozidi kunawiri kwa sasa. Roho Mtakatifu anatuita sote ili kufanya kazi kwa ushirikiano na ” kujenga uanajamii na umoja,” na hakika huo ni wito ambao Jukwaa Tendaji la Laudatio Si’ linafurahia kuutikia na kuujibu. (LS 149)
Tarehe 4, Oktoba imesalia kuwa siku ya thamani kuu katika kanisa na katika safari yetu pamoja, ndiyo siku tunayomsherehekea Mtakatifu Fransisiko wa Asisi, ambaye “anatualika kuyatazama maumbile kama kitabu cha maajabu anachotumia Mungu kusema nasi.” (LS 12) Ili kuadhimisha siku hii, na kutusaidia kimaombi katika matayarisho yetu kwenye safari iliyo mbele yetu, tunakualika ili kujiunga nasi katika siku arubaini (40) za maombi kwa ajili ya jamii ulimwenguni kote zinazosafiri nasi pamoja katika Laudato Si’.
Tafadhali jione huru kupakua ombi binfasi kwa kusudi la idara / sekta yako hapa.
Umekubaliwa kwa moyo wa mapendo kusambaza maombi haya miongoni mwa wenzako.
Maktaba (ya mapema) amilifu ya nyenzo na orodha ya hafla anuwai, vyote kwa ukarimu vitatolewa kuanzia tarehe 4 Oktoba, na mfumo wa mashirika ya wambia ambao ni wahusika-wenza katika kulibuni Jukwaa Tendaji la Laudato Si’. Tafadhali zitumie nyenzo hizi huru huria wako kwa kubofya kwenye kurasa za Nyenzo na Hafla.
Ni ombi kuu la Wanajukwaa Tendaji la Laudato Si’ kwamba kipindi kilichorefushwa cha maandalizi kitakuwa cha kupiga darubini na cha baraka tele, huku tukiungana kama familia moja ya Kikatoliki kwenye safari yetu ya uhimilivu katika moyo mkuu wa Laudato Si’.