Sajili

Mnamo tarehe 14, Novemba, Siku ya Maombi kwa Wanyonge Ulimwenguni, Wizara ya Maendeleo Muhimu ya Kibinadamu itaanzisha zoezi la kutoa Miongozo ya Laudato Si’ ya Kupangilia.

Kwa kujaza fomu hii ya usajili, unaahidi kujitolea kwako katika kuukuza Mpango wako wa Luadato Si’.

Miongozo ya Laudato Si’ ya Kupangilia hukuwezesha kutambua na kutekeleza itiko lako kwa Laudato Si’ kupitia mbinu za kimfumo.

Miongozo hii hujumuisha nyenzo za utambuzi na kutafakari, pia huwa na mwongozo kuhusu shughuli zenye athari chanya kwa lengo la kukutimizia Shabaha za Laudato Si’.

Plani zenyewe hutoa namna za kuyafuatilia na kuyatambulisha maendeleo yako.

Kuhusu mchakato

Mambo ya kutarajia

Kanisa la kila wote na “wake kwa waume wenye nia njema,” wanaongoza katika mabadiliko ya kimila ambayo ulimwengu unayahitaji mno.

Kwa kuijaza fomu ya usajili iliyotolewa awali, unaahidi kujitolea kwako kwa kusudi la kubuni Plani au Mpango wa Laudato Si’.

Mnamo tarehe 14, Novemba, Siku ya Maombi kwa Wanyonge Ulimwenguni, Wizara ya Maendeleo Muhimu ya Kibinadamu itaanzisha zoezi la usajili wa Plani au Mipango ya Laudato Si’.

  1. Zungumza na wengine katika jamii yako kuhusu Mipango ya Laudato Si’, kwa kutumia nyenzo ulizopewa.
  2. Hadi 14, Novemba, hitimisha kujitolea kwako na kuahidi kukamilisha mpango wako.
  3. Kuanzia 14, Novemba, kamilisha usajili wa mpango wako.

“Ni vyema kwa ubinadamu na ulimwengu wote kwa jumla wakati sisi waumini tutakapokutambua vyema kujitolea mhanga kwetu kiikolojia ambako chimbuko lake huwa imani zetu.”

(LS 64)

Shukran kwa moyo wa kupenda kufahamu mengi zaidi kuhusu Jukwaa Tendaji la Laudato Si'

Tunayo furaha kuu kuwa nawe katika safari hii.

Kwa umoja ndani ya Roho Mtakatifu na kwa himizo la upendo tunaoshiriki pamoja, tunatazamia kuwa pamoja katika hatua zetu zijazo.