Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Habari muhimu
Hii tovuti ni mahali kwa ajili ya jukwaa la hatua vitendo la Laudato Si’
Jukwaa la hatua za Laudato Si’ yatazinduliwa kwa awamu,na ujio wa kwanza mnamo Mei 2021. Taarifa Zaidi kuhusu hizi awamu na ratiba ya ujumla iko hpa.
Wizara ya Kuendeleza Umuhimu wa Maendeleo ya Binadamu inawakaribisha Kanisa Katoliki Ulimwenguni na “watu wote wenye mapenzi mema” kwenye mradi wa kujali Dunia yetu na kila mmoja wetu.
Wote ambao wanaanza safari yao ya Laudato Si’ na wale ambao wamekuwa wanachama hai kwa miaka mingi wote wanakaribishwa kujiunga. Jukwaa limeundwa katika ngazi zifuatazo:
- Familia
- Parokia na Majimbo
- Taasisi za elimu
- Mahospitali na vituo vya huduma ya afya
- Mashirika na makundi ( mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), walei, ikolojia ya jamii, miradi, sekta za mawasiliano)
- Vyombo vya uchumi ( mashamba, vyama vya ushirika, biashara)
- Mashirika ya dini (Mapadre na watawa, majimbo, jamii)
Vyema kabisa! Hamu yako katika kujitolea ni ishara kwamba upo tayari kwa safari ya kuitambua ikolojia fungamano.
Wewe ndiwe utakayeibuni Plani yako ya Laudato Si’ madhali ndiwe mtaalamu katika mahitajika binafsi na vipaumbele.
Mwongozo wa Plani upo tayari ili kukuelekeza wewe. Unashughulikia mbinu imara na fafanuzi, kipindi cha tafakari, kuteua hatua za kuchukua na kutathmini maendeleo.
Wale ambao hujiunga nasi hupata fursa ya kufikia orodha ya hatua-pendekezo zilizolengwa kwa idara/sekta na meaneo yao, njia za tathmini-binafsi ili kuwa kielelezo cha maendeleo ya mwaka, na muungano na wambia wa mradi huu kote ulimwenguni.
Hatua/vitendo vyote vinakaribishwa.
Washiriki wanahimizwa kufanya maendeleo kuelekea Malengo ya Laudato Si’ katika kipindi kisichozidi miaka saba. Habari Zaidi zinapatikana hapa.
Miongozo ya Laudato Si’ ya Kupangilia hukuwezesha kutambua na kutekeleza itiko lako kwa Laudato Si’ kupitia mbinu za kimfumo.
Miongozo hii hujumuisha nyenzo za utambuzi na kutafakari, pia huwa na mwongozo kuhusu shughuli zenye athari chanya kwa lengo la kukutimizia Shabaha za Laudato Si’. Plani zenyewe hutoa namna za kuyafuatilia na kuyatambulisha maendeleo yako.
Taarifa za kina kuhusu Mipango ya Laudato Si’ zitachapishwa katika mwezi wa Novemba.
Masharti ya kawaida
Jukwaa la hatua vitendo la Laudato Si’ ni ratiba mipango na kwa kutumia tovuti inayo saidia kuwapatia taasisi za katoliki na jamii , na familia kutekeleza mafunzo ya Laudato si’. Inafadhiliwa na Wizara ya Vatikani ya kukuza maendeleo ya binadamu, na imeendelezwa kwa mbinu ya kutoka chini hadi juu kwa kushirikiana na wakatoliki na taasisi mbalimbali. Inatoa muongozo na nafasi kwa wote kushirikiana ki mawazo, kuuliza maswali, kuangalia changamoto, na dira mpya, kwakuwa ‘’vyote ni vikubwa zaidi ya jumla ya sehemu zake.” (LS 141)
Malengo ya Laudato Si’ ni kituo chetu cha safari. Yanatoa muongozo katika kufanikisha ikolojia ya mafundisho jamii/mazingira. Taarifa Zaidi ziko hapa
Miongozo ya Laudato Si’ ya Kupangilia hukusaidia kutambua na kutekelezea itiko lako kwa Laudato Si’ kupitia mbinu za kimfumo zilizotoholewa kwa mujibu wa matakwa ya taasisi yako, jamii au familia yako.