“Talanta na ushiriki wa kila mtu unahitajika "( Laudato Si '14 )

Chukua hatua halisi katika utunzaji wa dunia makao yetu ya kawaida. Jukwaa Tendaji la Laudato Si' linatoa zana na rasilimali kwa Kanisa katika safari kwenye uendelevu kamili katika ari ya ikolojia fungamano.

Jiandikishe

KUHUSU JUKWAA HILI

Jukwaa Tendaji la Laudato Si’, ambalo ni mpango wa Wizara ya Vatikani ya Ukuzaji wa Maendeleo Muhimu ya Kibinadamu, limetiwa msukumo na waraka wa Papa Fransisko wa Laudato Si’,2015 . Linaliwezesha Kanisa kufikia suluhu za kweli na za kudumu kwa migogoro ya kiikolojia. Mpango huu unaokua kila wakati unasaidia washiriki kutayarisha Mipango ya Laudato Si’ iliyoelekezwa kutimiza lengo moja: Hatua za madhubuti ili kulinda nyumba yetu ya Pamoja.

Jifunze zaidi kuhusu jukwaa hili

Image decoration

“Kuna uungwana katika jukumu la kuyatunza maumbile kupitia kila hatua ndogo kila siku, na vyema zaidi jinsi elimu inavyoleta mabadiliko halisi katika mitindo ya maisha.”

(LS 211)

Shabaha za Laudato Si’

Athari Yetu

Kuelewa mahali tulipo safarini kwenye uhimilivu kamili katika dhati ya moyo jumlishi wa ikolojia fungamano ni muhimu ili kupiga hatua pamoja. Kila mwaka, washiriki katika Jukwaa Tendaji la Laudato Si’ hukumalisha tathmini-binafsi ya desturi au shughuli zao katika sehemu zilizodokezwa na Shabaha za Laudato Si’. Kuelewa mahali tulipo leo ndiyo hatua ya kwanza katika kuelewa tutakapoelekea kesho.

Jifunze zaidi

Anza safari

Mnamo tarehe 14, Novemba, Siku ya Maombi kwa Wanyonge Ulimwenguni, Wizara ya Maendeleo Muhimu ya Kibinadamu itaanzisha zoezi la kutoa Miongozo ya Plani za Laudato Si’.

Miongozo ya Laudato Si’ ya Kupangilia hukuwezesha kutambua na kutekeleza itiko lako kwa Laudato Si’. Taasisi yako, jumuia, au familia yako imealikwa mapema kujitolea katika mchakato wa mipango hii. Kwa kujaliza fomu ya usajili. , unaahidi kuiandama Mipango ya Laudato Si’ punde tu itatakapozinduliwa rasmi.

Umekaribishwa vyema kuzitumia nyenzo zifuatazo huku ukitafakari hatua za safari iliyo mbele yako.

Jiunge na mazungumzo

Jiandikishe kwa Jukwaa Tendaji la Laudato Si' ili kupokea Sasisho za baruapepe.

Jisajili uhamasishwe na vitendo halisi vya washiriki ulimwenguni kote na katika jamii yako. Pokea maoni juu ya njia ambazo unaweza kuchukua hatua mahali ulipo. Pata habari za hivi karibuni na matukio yanayoongozwa na taasisi, mashirika, na watu ulimwenguni kote katika utunzaji amilifu wa makao yetu ya pamoja.

"*" indicates required fields

“Tufundishe kugundua thamani ya kila kitu, kujawa na staha na kutafakari, kutambua kuwa pakubwa tumeunganishwa na kila kiumbe katika safari ya kuelekea kwenye mwanga wako wa milele.” (LS 246)

Sajili

STEERING BOARD

Maswali Vaulizwayo Mara Kwa Mara

Jukwaa Tendaji la Laudato Si’  hutoa msaada wa kina  safari hii kwenye ikolojia fungamano kama taasisi, jamii, au familia. Sehemu hii inatoa taarifa amilifu na mfano wa istilahi za kawaida.

Taarifa Zaidi